Majimbo matatu nchini Marekani yameruhusu baadhi ya maduka kufunguliwa tena baada ya hatua zilizowekwa za kukabiliana na kusambaa kwa virusi vya corona, huku idadi ya vifo nchini humo ikizidi watu 51,000.
Saluni za wanaume na wanawake sasa zinaweza kufunguliwa tena katika majimbo ya Georgia Oklahoma huku Alaska ikiondoa masharti iliyokuwa imewekea migahawa.
Ijumaa rais Donald Trump aliondoka mapema kuliko ilivyo kawaida wakati otuba yake ya kawaida kuhusu maendeleo ya hali ya janga la corona, akakataa kupokea maswali ya waandishi wa habari.
Rais Trump amekabiliwa na ukosoaji mkubwa baada ya kupendeza kuwachoma sindano ya kemikali za kuua vimelea au za usafi wagonjwa wa corona inaweza kuwa ni jambo la manufaa.
Kauli zake zimekua zikilaaniwa na madaktari pamoja na watengenezaji wa bidhaa wanaozitaja kuwa ni za hatari. Kemikali za kuua vijidudu au vimelea zinaua na zinaweza kuwa sumu zikiingizwa katika mwili wa binadamu , na hata matumizi yake ya nje ya mwili yanaweza kuwa hatari kwa ngozi, macho na mfumo wa kupumua.
Bwana Trump alisema siku ya Ijumaa kuwa kauli-alizozitoa katika mkutano wa wanahabari siku moja kabla zilikuwa za vichekesho na muktadha wake ulipotoshwa.
Je ni nini kinachoendelea katika majimbo hayo matatu?
Wateja wanaotembelea biashara mpya zilizofunguliwa katika majimbo ya Georgia, Oklahoma na Alaska watatarajiwa kuendelea kuheshimu hatua za kutosogeleana .
Lakini baadhi ya miji na maeneo wameamua kuendelea kutekeleza hatua yao ya kukaa nyumbani.
Katika jimbo la Georgia, ambalo lina moja ya ratiba ya haraka sana ya kufungua shughuli nchini humo ,saluni za wanaume na wanawake, za kutengeneza kucha , tatuu, na biashara nyingine za mapodozi zitaruhusiwa kufungua shughuli zake.
Siku ya Jumatatu migahawa ya chakula na kumbi za michezo zitaruhusiwa kufunguliwa tena.
Huku kukiwa na madai ya ukosefu wa ajira kwa watu milioni 26-au takribani 15% ya watu wa Marekani - tangu katikati mwa mwezi Machi, majimbo menfufua biashara zilizositishwa kutokana na janga la corona.
Lakini wataalamu wa afya wameonya kuwa hatua hizo huenda zikawa zimechukuliwa mapema, huku kukiwa na hofu kwamba zinaweza kusababisha wimbi jingine la maambukizi.
Baada ya kukosolewa na Trump,Gavana wa jimbo la Georgia Brian Kemp amri kali za usafi na watu kutosogeleana kuhusu kuhusu migahawa.
Je ni yapi zaidi yaliotokea Ijumaa?
Katika hotuba ya White House iliyodumu kwa muda wa dakika 20,Bwana Trump aliwaomba watu kuendelea kufuata sheria zinazohusu kutotengamana kwa watu katika jamiina kutumia barakoa.
Pia Ijumaa, Bwana Trump pia alisaini muswada wa thamani ya bilioni 484 (Pauni Bilioni 391) za kuchochea uchumi , akisema kuwa anataka "kuharakisha nafuu ya kiuchumi kwa ajili ya raia wetu".
Ni msaada wan ne wa Covid-19 ikupima virusi, hospitali na mpango wa mikopo ya biashara ndogondogo.