Dhoruba yapelekea vifo vya watu 7 Marekani

Watu 7 wamepoteza maisha katika majimbo matatu kutokana na dhoruba kusini mashariki mwa Marekani.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na Huduma ya Hali ya Hewa ya Taifa, imegundulika kuwa dhoruba hiyo, iliyosababisha vifo vya watu 7 katika majimbo ya Oklahoma, Texas na Louisiana, iliendelea jana katika majimbo ya Mississippi, Alabama na Florida.

Zaidi ya Wamarekani 150,000 kati ya Texas na jimbo la Georgia pia wameripotiwa kutokua na umeme kutokana na dhoruba.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items