Dkt. Ndumbaro amewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari ya corona



Na Muhadh Mohammed, Songea Ruvuma.

Naibu waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika mashariki Dkt. Damasi Ndumbaro amewataka wana nchi kuendelea kuchukua tahadhari kujikinga na ugonjwa wa covid19
unao sababishwa na virus vya corona kwakua mpaka sasa ugonjwa huo haujapata tiba.

Dkt. Ndumbaro ameongeza kuwa serikali itaendelea na utaratibu wa kuweka Karantini watu wote watakao hisiwa kuwa na maambukizi pamoja na wale wanao ingia nchini kutoka nchi za nje ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo huku akiwataka watanzania kuchapa kazi.

Katika hatua nyingine Dkt. Ndumbaro ametoa msaada wa computer na printer katika shule ya Sekondari Siri ,pamoja na computer katika shule za sekondari Londoni,Ruvuma, Songea girls pamoja na Songea boys ili ziweze kuwasaidia waalimu kuweza kutoa elimu kwa ubora.


Akishukuru kwa niaba ya waalimu wa shule za sekondari zilizo pokea msaada huo mwalimu mkuu wa shule ya sekondari siri Christopher Banda amesema computer hizo zitaondoa kero ya kutembea mda mrefu kufuata huduma za kuchapisha mitihani pia itasaidia kuwa mazoezi ya mara kwa mara wanafunzi na kufanya vizuri kitaaluma.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items