Idadi ya vifo vya COVID-19 yakaribia 200,000 duniani


Idadi vifo duniani vilivyosababishwa na virusi vya corona inakaribia 200,000 wakati Umoja wa Mataifa ukizindua mpango wa ulimwengu wa kutafuta chanjo dhidi ya janga hilo la kimataifa.

Serikali duniani zinajaribu kudhibiti msukosuko wa kiuchumi uliosababishwa na virusi vya corona ambavyo tayari vimewakumba kiasi watu milioni 2.8 na kulazimisha wengine kubakia chini ya vizuizi vikali.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amewataka viongozi duniani, masharika ya kimataifa na sekta binafsi kujiunga aktika juhudi za kutafuta chanjo akisema ulimwengu unakabiliwa kitisho kisicho na mfano.

Wakati wa mkutano uliofanyika kwa njia ya video na kuhudhuriwa na viongozi wa Ufaransa na Ujerumani, Guetteres amesisitiza kuwa chanjo dhidi ya virusi vya corona inapaswa kuwa salama, nafuu na itakayopatikana kwa wote.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items