Idadi ya walioambukizwa virusi vya Corona India yaongezeka kwa kasi


India imerekodi ongezeko kubwa la kesi za maambukizi ya virusi vya Corona kwa siku moja leo Jumatatu wakati serikali ikianza kuchukua hatua ya kulegeza vizuizi vilivyowekwa kuzuia kuenea kwa maambukizi.

Vizuizi hivyo vinalegezwa kuruhusu shughuli za utengenezaji bidhaa na kilimo kuanza kazi.

 Katika kipindi cha saa 24 India imerekodi kesi 1,553 za maambukizi na kuifanya idadi jumla ya walioambukizwa virusi vya Corona nchini humo kufikia watu 17,000.

Takriban watu 543 wameshakufa kutokana na ugonjwa wa Covid-19 nchini humo na wataalamu wa magonjwa ya mripuko wametabiri kwamba kilele cha maambukizi nchini India kitafikiwa mwezi Juni.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items