Rais wa Iran Hassan Rouhani, amesema shughuli za kiuchumi ambazo si hatari zitarejea tena kuanzia Aprili 11 katika taifa hilo la Mashariki ya Kati lililoathiriwa pakubwa na virusi vya Corona.
Iran imekuwa ikipambana kudhibiti kusambaa kwa virusi hivyo vinavyoshambulia mfumo wa kupumua na kusababisha ugonjwa wa COVID 19.
Serikali ya nchi hiyo hata hivyo ina wasiwasi kuwa mikakati ya kudhibiti ugonjwa huo huenda ikalididimiza kiuchumi taifa ambalo tayari linakabiliwa na vikwazo vya kiuchumi.
Rouhani amesema chini ya usimamizi wa wizara ya afya, shughuli hizo zitaanza kuanzia siku ya Jumamosi ijayo isipokuwa mjini Tehran, akisema thuluthi mbili ya wafanyakazi wa serikali watafanyia kazi nyumbani.
Rais Rouhani hata hivyo hakufafanua ni shughuli za aina gani alizoziorodhesha kama shughuli zilizo na "hatari ndogo."