Kansela Merkel atoa wito wa ushirikiano wa kimataifa dhidi ya virusi vya corona

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ametoa wito wa ushirikiano wa kimataifa kuhusu utafiti wa chanjo ya virusi vipya vya corona, akisema janga hilo halichagui mipaka na linaweza tu kukabiliwa kwa pamoja.

Akizungumza bungeni jana, Merkel alisema wanasayansi wa Ujerumani wanafanya utafiti usiku na mchana kuhusu kirusi hicho, lakini ushirikiano wa kimataifa dhidi ya kirusi hicho ni muhimu sana. Merkel amesema sayansi sio ya kitaifa tu, bali ni ya wanadamu wote.

Kwa hivyo wakati dawa au chanjo inapopatikana, kujaribiwa, na kuruhusiwa tayari kwa matumizi, lazima ipatikane kote duniani na kwa bei nafuu. Kansela amesisitiza kuwa Ujerumani inashirikiana kikamilifu na kuliunga mkono Shirika la Afya Duniani - WHO katika utekelezaji wa majukumu yake.

 Ujerumani wiki hii ilianza kuondoa baadhi ya vizuizi baada ya kusitisha shughuli kwa wiki kadhaa, huku ikiyaruhusu maduka madogo madogo kuanza kufungua biashara zao.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items