Siku ya jana Ijumaa Aprili 3, 2020 ilitolewa taarifa ya kusogezwa mbele pambano la ngumi kati ya Muingereza Anthony Joshua na Mbulgaria Kubrat Pulev, ambalo lilipangwa kufanyika Juni 30, 2020 kwenye uwanja wa Tottenham.
Taarifa ya kusogezwa mbele kwa pambano hilo, ilitolewa na promota wa Anthony Joshua Matchroom Boxing, ambapo alisema tarehe mpya itapangwa tena kutegemeana na mwenendo wa janga la Corona.
Hii inakuwa mara ya pili kwa wawili hao pambano lao kuingia dosari ambapo, Joshua na Pulev walitakiwa kupigana tangu mwaka 2017 kuwania mkanda wa dunia wa IBF lakini ikashindika.
Pulev mwenye miaka 38, alilazimika kujitoa wiki mbili kabla ya pambano hilo kupigwa kwenye uwanja wa Manispaa ya Cardiff, kutokana na kupata majeraha ya bega wakati akifanya mazoezi ya kujiandaa na pambano.
Pambano la sasa ni la kuwania ubingwa wa dunia katika uzito wa juu ambapo Joshua atakuwa analinda mikanda yake minne ya IBF, WBA, WBO na IBO.