Na Rebeka Duwe, Tanga.
Mkuu wa mkoa wa Tanga Martini Shigela amewataka wananchi wa mkoa kuzingatia maagizo ya wataalamu wa afya ili kuweza kujikinga na ugonjwa wa Corona ambao ni janga la Dunia na kwamba kuchukua tahadhari ya kunawa mikono na kuepuka msongamano usio wa lazima na safari ambazo si lazima.
Hayo aliyasema wakati akipokea msaada wa matanki matano ya maji tiririka yenye Dawa kwa ajili ya kunawa mikono yaliyotolewa na kampuni ya mafuta PPTL kwa lengo la kuunga juhudi za serikali za kupambana na magonjwa ya Corona katika standi ya magari iliyopo Ngamiani kata ya Ngamiani kati.
Aidha aliwashukuru kampuni hiyo kwa kuliona hilo kwamba wameweza kuliunga mkono juhudi za serikali lakini pia kuona umuhimu wa kutoa matanki hayo kwa ajili kupambana na ugonjwa huo kwa kuwahimiza wananchi kunawa mikono wanaingia standi na kwenye usafiri wa daladala.
Aliongeza kusema kuwa sio lazima watu kutoka majumbani kwao kwa ajili ya kuzunguka mjini kama hakuna kazi maalumu ya kufanya ingefaa kukaa kwake na familia yake ili kujiepusha na maambukizi ya ugonjwa huo ambao ni hatari kwa kila mtu .
Hata hivyo baadhi ya wananchi wa walipongeza juhudi za serikali za kuhamasisha uzingatiaji wa maagizo ya wataalamu wa afya pamoja na serikali na kuiona serikali kuzidi kutoa elimu ya uzingatiaji wa magizo hayo hadi maeneo ya pembezoni mwa mji.
Aidha waliongeza kusema kwamba zipo kero kwa baadhi ya magari ambayo yanazidisha abiria tofauti walivyoshauriwa na serikali kwamba watu wasiewe na msongamano kwenye daladala hivyo ni vyema elimu hiyo ikaendelea kutolewa kwa msisitizo zaidi ili kujiepusha maradhi hayo.