Idadi ya maambukizi mapya ya virusi vya Corona nchini Marekani imepanda na kufikia zaidi ya watu 300,000 hapo jana huku zaidi ya vifo 8,175 vitokanavyo na matatizo yanayohusiana na ugonjwa wa COVID 19 vikiripotiwa.
Rais wa Marekani Donald Trump ameonya kuwa wiki zijazo huenda zikawa ngumu zaidi kwa taifa hilo.
Akizungumza katika ikulu ya White House, Trump amesema taifa hilo litashuhudia idadi kubwa sana ya vifo wiki zijazo huku akisisitiza umuhimu wa kurejea makazini, ingawa hakutaja tarehe rasmi.
Zaidi ya watu milioni 10 nchini humo wamepeleka maombi ya bima ya kutokuwa na ajira katika kipindi cha wiki mbili za mwisho za mwezi Machi hatua inayoashiria kiwango halisi cha watu wasio na ajira kikiwa kimepitiliza asilimia 10, huku kukitarajiwa athari zaidi wakati taifa hilo likikabiliana na virusi vya Corona.