China kutuma ujumbe Israel baada ya balozi wake kufariki

China itapeleka ujumbe wake nchini Israel baada ya balozi wake mjini Tel Aviv Du Wei kukutwa amekufa nyumbani kwake jana Jumapili.

Taarifa hiyo imeelezwa leo na wizara ya mambo ya nje ya Israel. Msemaji wa wizara hiyo, Lior Haiat ameliambia shirika la habari la Kijerumani, dpa kwamba ujumbe huo wa China umedhamiriwa kwenda kusaidia katika shughuli ya mipango ya kuusafirisha mwili wa mwanadiplomasia huyo nyumbani China.

Hata hivyo, msemaji huyo wa wizara ya mambo ya nje ya Israel hakuthibitisha ripoti iliyoandikwa kwenye gazeti la Haaretz kwamba ujumbe huo wa China utafanya uchunguzi kuhusu mazingira ya kifo cha balozi wake huyo.

 China haina mamlaka ya kisheria kufanya uchunguzi nchini Israel. Huduma ya matibabu ya Israel ya Magen David Adom ilisema jana kwamba balozi huyo wa China mwenye umri wa miaka 58 inaonesha alifariki kutokana na mshtuko wa moyo.

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia