Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Duniani WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema tathmini huru ya jinsi janga la kirusi cha corona linavyoshughulikia itaanzishwa haraka iwezekanavyo na China imeunga mkono hatua hiyo.
Mkuu huyo wa WHO ametoa ahadi hiyo wakati wa mkutano wa wa baraza kuu la shirika hilo uliofanyika kwa njia ya kidijitali ambapo rais wa China, Xi Jinping aliitetea nchi yake kuhusu ilivyoushughulikia mgogoro huu.
Rais wa Marekani Donald Trump amehoji utendaji wa WHO wakati wa janga hili na kuongoza ukosoaji wa Jumuiya ya Kimataifa kuhusu hatua zilizochukuliwa na China kushughulikia suala hili katika kipindi cha mwanzoni kabisa cha mgogoro huu.
Aidha katika mkutano huo ulioratibiwa kutokea makao makuu ya WHO mjini Geneva,Kansela wa Ujerumani Angela Merkel kwa upande wake amesema nchi zinahitaji kushirikiana kulishinda janga hili na kwamba hakuna nchi inayoweza kulitatua tatizo hili peke yake.
Kadhalika wanachama wa shirika hilo wamekubaliana katika mkutano huo kuahirisha mjadala kuhusu kuipa nafasi Taiwan ya kuwa mwanachama muangalizi.Uamuzi huo umefikiwa licha ya Marekani na nchi nyingine kuzidisha shinikizo katika siku za karibuni kutaka Taiwan ikubaliwe.