Hizi ndio sababu zinazopelekea biashara nyingi kufa



Tafiti zinaonyesha biashara nyingi zinazoazishwa leo huwa hazina maisha marefu sana. Biashara nyingi huwa haziwezi kufikisha miaka kumi, hii ni kutokana na wingi wa changamoto zinazopatikana  katika biashara hizo.

Zifuatazo ndizo sababu za biashara nyingi kufa;

1. Haikulenga kutatua tatizo maalumu.
Imeanzishwa sababu muhusika ameipenda ameona anaiweza ila hakukuwa na soko linaloihitaji, inawezekana kuna wanaoifanya vizuri zaidi au kuna kuna mbadala wake tofauti.

2. Bidhaa zipo chini ya kiwango
Inaweza kuwa inahitajika sana ila ukaipekeka kwa wateja ikiwa chini ya kiwango kinachotakiwa. Mteja anapolipia bidhaa anataka ikidhi mahitaji yake na matazamio yake nje ya hapo hawezi kurudi tena.


3. Kuzindua wakati usio sahihi
Kuna biashara ambazo muda sahihi ni muhimu sana. Mfano anataka kuuza vifaa vya shule, muda muafaka sio wanapokaribia kufunga shule bali kufungua. Ukitaka biashara mpya ijulikane kwa urahisi izindue katika muda sahihi.


4. Kutokuthamini wateja
Watu wanasahau kuwa mteja ndio anakuweka sokoni. Kupuuzia malalamiko, ushauri na mawazo ya wateja na kuwafanya wajisikie hawahitajiki kutasababisha madhara kwenye biashara yako. Lazima wateja wathaminiwe.

5. Upangaji mbaya wa bei
Bei zinatakiwa kupangwa kutokana na gharama za uendeshaji na faida. Unapoweka bei juu sana sababu gharama zako zipo juu au chini sana kuliko gharama zako ili uvutie wateja unajikuta haufikii malengo ya faida na hivyo bishara inashindwa kusimama.

6. Kupoteza Muelekeo
Unaanza biashara katikati unasahau ulipokuwa unaelekea unajikuta upo upo tu au umebadili mwelekeo bila mipango, lazima ushindwe kuendelea.