Janga la corona, Serikali ya Ivory Coast imeruhusu vyuo na shule kufunguliwa na tayari wanafunzi wamerudi darasani huku tahadhari zikiendelea kuchukuliwa ili kuzuia maambukizi ya virusi hivyo.
Ivory Coast inakuwa Nchi ya kwanza Afrika Magharibi kuruhusu masomo kuendelea baada ya takribani miezi miwili ya lockdwon”mwanzoni tulikuwa na hofu lakini sasa tumeona kawaida, tahadhari zinachukuliwa na maisha lazima yaendelee”
Tanzania imeruhusu pia wanafunzi wa vyuo na wale wa kidato cha sita kurudi darasani kuanzia June 01,2020 na jana Waziri wa Elimu Prof. Joyce Ndalichako ameutangaza rasmi mwongozo wa Wizara ya Afya uliosainiwa na Waziri Ummy Mwalimu ummy Mwalimu ukilenga kudhibiti corona pindi wanafunzi wanaporudi kuendelea na masomo.