Kansela Merkel atoa wito wa mshikamano wa Ulaya na Ulimwengu

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema Umoja wa Ulaya unapaswa kuchukua jukumu la mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya virusi vya corona duniani katika wakati mahusiano ya kanda hiyo na Marekani yamekuwa magumu.

Katika hotuba yake aliyoitoa kuzungumzia vipaumbele vya Ujerumani itapochukua uenyekiti wa zamu wa Umoja wa Ulaya mnamo mwezi Julai, Merkel ameitaka Ulaya kuonesha mshikamano zaidi na ulimwengu.

Amesema Ulaya hatupaswi kusahau msimamo wake wa kuegemea siasa za magharibina inatakiwa kuwa washirika wa kutumainiwa wa misingi na maslahi ya magharibi duniani Katika hotuba hiyo Merekal pia amelikaribisha pendekezo la Umoja wa Ulaya wa kuanzisha mfuko wa uokozi wa dola bilioni 750 kusaida kukabiliana na athari za viruis vya corona na kusema msaada zaidi unapaswa kutolewa.

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia