Taiwan yaahidi kuwapa hifadhi wanaokimbia Hong Kong

Taiwan imeahidi leo kuwakaribisha wakaazi wa Hongkong wanauoukimbia mji huo ulio chini ya himaya ya China kwa sababu za kisiasa wakati Beijing ikijaribu kupitisha sheria mpya ya usalama kwenye mji huo iliyozusha maandamano mapya.

Mkuu wa sera ya Taiwan kuhusu China Chen Ming-tong ameliambia bunge mjini Taipei kuwa serikali itaanzisha taasisi ya kutoa msaada wa kiutu kwa wakaazi wa Hong Kong utakaojumuisha nyumba za kuishi na ajira kwa kushirikiana na makundi ya wanaharakati,.

Wiki iliyopita rais wa Taiwan Tsai Ing-Wen alikuwa kiongozi wa kwanza duniani kuahidi hatua mahsusi za kuwasaidia watu wa Hongkong wanaotaka kuuhama mji huo kutokana na sheria mpya ya usalama.

Uamuzi huo utalemaza zaidi mahusiano kati ya China na Taiwan ambayo katika siku za karibuni imekuwa kituo muhimu kwa wakaazi wa Hong Kong wanaoukimbia mji huo.

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia