May 26, 2020

Kuhusu ligi kuchezwa kituo 1,klabu yamuomba Waziri

Baadhi ya klabu za Ligi Kuu Tanzania bara zimeonekana kulalamikia gharama zitakazojitokeza pindi ligi itakapoendelea kwa kuchezwa katika kituo kimoja cha Dar es Salaam.


Hatua hiyo inakuja kufuatia Rais Magufuli kutoa ruhusa ya ligi kurejea na siku kadhaa baadaye Waziri wa Sanaa, Habari, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe kutoa utaratibu wa namna ligi itachezwa, akiitaja Dar es Salaam kuwa ni mkoa kwa ajili ya Ligi Kuu.

Afisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire ni miongoni mwa waliotoa maoni yao katika hatua hiyo ambapo amesema kuwa utaratibu wa kucheza ligi katika kituo kimoja utaziathiri zaidi klabu za mikoani kiuchumi kutokana na gharama za kuweka kambi kwa mwezi mmoja.

Masau Bwire amesema gharama ya kuweka kambi katika hoteli kwa timu moja kwa mwezi mzima siyo chini ya Sh. milioni 58 kwa mwezi mzima, jambo ambalo si rahisi kwa klabu nyingi hasa za nje ya Dar es Salaam, hivyo amemuomba Mhe. Waziri kukaa na wadau kuweka utaratibu mzuri kwa klabu hizo.

Mapema kabla ya ruhusa ya kuendelea ligi kutolewa na Rais Magufuli, klabu ya Ndanda ililalamika kukosa pesa za kuendesha klabu hasa kutokana na madhara ya COVID-19 na kuiomba Bodi ya Ligi na TFF kutoa msaada, na baadaye Bodi ya Ligi ilijibu kuwa haina pesa za kuzisaidia klabu na badala yake wataziwahisha pesa za wadahamini wao.

KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger