Madiwani 8 wa chama cha CUF watimkia CCM

Madiwani 8 wa kata 8 za wilayani Tunduru pamona na kada maarufu KIOSA KIOSA wameachana na Chama Cha Wananchi CUF na kujiunga na CCM asubuhi hii.

Madiwani hao wote 8 wamepokelewa na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho na viongozi mbalimbali wa mkoa na wilaya.

Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Ndg. Julius Mtatiro ambaye ni mjumbe wa kamati ya siasa ya wilaya ya Tunduru amethibitisha taarifa hizo.

Madiwani hao wanatokea kata za Majengo, Nalasi Magharibi, Nandembo, Mlingoti Mashariki, Ligunga, Tinginya na Nakapanya.

Wakizungumza mbele ya Mwenyekiti wa CCM wa mkoa, madiwani hao wamesema kuwa wamefanya uamuzi huo kwa sababu wanahitaji chama imara kitakachowasaidia kutumikia wananchi kwa utulivu na mienendo inayooeleweka.

Madiwani hao wamefanya maamuzi hayo ikiwa ni miezi michache toka Chama cha Wananchi CUF kigawanyike na baadhi ya makada maarufu kuhamia ACT na CCM.

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items