Serikali mpya ya mseto ya Israel yala kiapo


Bunge la Israel limeiapisha serikali mpya ya mseto itakayoongozwa na waziri mkuu Benjamin Netanyahu pamoja na mpinzani wake Benny Gantz. Hatua hiyo inahitimisha mzozo wa kisiasa ambao haukuwahi kushuhudiwa kwenye historia ya taifa hilo.

 Wabunge waliiidhinisha serikali hiyo itakayoongozwa kwa miaka mitatu kwa kura 73 dhidi ya 46 za waliopinga na mbunge mmoja hakuhudhuria. Bunge la Israel lina viti 120.

 Serikali hiyo mpya inayoingia baada ya siku 500 za kutokuwepo na serikali thabiti imejiandaa kukabiliana na mizozo mikubwa katika wiki zake za mwanzo ikiwa ni pamoja na kuanguka kwa uchumi kulikosababishwa na janga la virusi vya corona.

 Rais wa Urusi Vladimir Putin na waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Mike Pompeo wamekaribisha na kupongeza hatua hiyo.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items