Siri ya kutua ndege ya utawala haramu wa Kizayuni kwenye ardhi ya Sudan, yafichuka



Ndege ya utawala haramu wa Israel ambayo hivi karibu ilitua katika ardhi ya Sudan, ilikuwa na lengo la kumuokoa dalali anayefuatilia kuboreshwa uhusiano wa nchi hiyo na Tel Aviv ambaye alikuwa ameambikizwa virusi vya Corona.

Habari kutoka nchini Sudan zinasema kwamba Najwa Qadeh al-Dam, mshauri wa Abdel Fattah al-Burhan, Mkuu wa Baraza la Utawala nchini Sudan alifariki dunia siku ya Jumatano kutokana na ugonjwa wa Covid-19. Kwa mujibu wa habari hiyo siku ya Jumanne ndege moja ya utawala wa Kizayuni ya shirika la Arrow, ambayo kwa kawaida hutumika kwa ajili ya masuala ya dharura ilitua katika uwanja wa ndege wa Khartoum ikiwa na timu ya madaktari kwa lengo la kumsafirisha Najwa Qadeh al-Dam kuelekea ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) kwa ajili ya matibabu, ingawa alifariki dunia katika hospitali ya Alyau, ya mjini Khartoum.


Gazeti la Al-Sudani limezidi kufafanua kuwa Qadeh al-Dam alitajwa kama mmoja wa watu walioratibu kikao cha mwezi Februari iliyopita kati ya Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa Utawala Haramu wa Israel na Abdel Fattah al-Burhan, Mkuu wa Baraza la Utawala nchini Sudan huko nchini Uganda. Mawakili kadhaa wa Sudan wamemfungulia mashtaka ya jinai Al-Burhan kwa sababu ya kukutana na waziri mkuu huyo wa utawala haramu wa Israel.

Aidha chama cha Kongresi ya Watu wa Sudan kilitoa taarifa kikiitaja hatua ya Al-Burhan ya kukutana na Netanyahu kuwa ni ya kufedhehesha. Katika miezi ya hivi karibuni utawala bandia wa Kizayuni umezidisha juhudi za kupanua uhusiano wake na nchi za Afrika hususan zilizo na utajiri wa mafuta na madini kama vile ya almasi, urani na dhahabu.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items