Loading...

5/22/2020

Taasisi ya kiislam ya wipahs yakabidhi vifaa vya usafi hospitali ya wilaya ya kondoa

Taasisi ya kislam ya world islamic propagation and humanitarian services (wipahs) chini ya Chini ya mwenyekiti wake Mzee Hajj Swahibu kushirikiana na tanzania ithnaashary community T.I.C. Imekabidhi idadi ya vitanda kumi (10).

Sheikh Abdullatwif swalehe Akikabidhi vifaa ivyo mbele ya mganga mfawidhi dr francis Mwita saghat, Aidha upande wake mganga mfawidhi ameshukuru Taasisi ya WIPAHS kwa ushirikiano waliounesha wa kutoa msaada katika hospital hiyo huku akisema ni kwa miaka mitano yuko hapa hospital hawajawahi kupokea msaada wa aina hiyo.


Akizungumza kwa niaba ya taasisi ya wipahs shekhe Abdullatuf swalehe amesema msaada huo wa kibinaadamu uliotolewa ni katika harakati za kuunga Mkono juhudi za serikali ya jamhuri ya muungano wa tanzania chini ya rais wake mh John Pombe Magufuli juu ya mapambano dhidi ya ugonjwa wa mapafu unaosababishwa na na virusi vya corona.
KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger