TANZIA : BABU NJENJE AMEFARIKI DUNIA

Taarifa iliyoifikia asubuhi hii inaeleza kuwa, Mwanamuziki mkongwe wa Bendi ya Kilimanjaro maarufu kama wana njenje, Mabrouk Hamis Omar almaarufu kama  Babu Njenje amefariki dunia leo jijini Dar es salaam baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Akizungumza nasi kwa njia ya simu, Mmoja wanamuziki wa bendi hiyo, John Kitime amesema "Ni kweli Babu Njenje amefariki na sasa naelekea pale alipokuwa akiishi, Mtaa wa Mindu Upanga ambapo taratibu zitafanyika".

Babu Njenje atakumbukwa kwa nyimbo zake nyingi zikiwemo Njenje, Kinyaunyau na nyingine nyingi.

Taarifa zaidi tutawaletea hapo baadae.

Inna lillah wainna ilaih rajiun.