Umoja wa Ulaya umeelezea wasiwasi mkubwa hii leo juu ya sheria ya usalama ya China kwa ajili ya Hong Kong.
Hayo yamesemwa na mkuu wa sera za kigeni wa umoja huo, Josep Borrell, baada ya mkutano wa mawaziri 27 wa kigeni wa kanda hiyo.
Borrel amesema hatua hiyo kwa kiasi kikubwa inahatarisha kudhoofisha msingi wa taifa moja, mifumo miwili.
Amesema, mahusiano ya Ulaya na China yanajikita katika kuheshimiana na kuaminiana, lakini uamuzi huo unaibua mashaka.
Jijini Hong Kong, kumeibuka maandamano mengine hii leo kufuatia kura ya bunge la China ya kuidhinisha sheria hiyo mpya ya usalama itakayodhibiti vikali shughuli za siasa za upinzani na mashirika ya kiraia katika jiji hilo ambalo ni kitovu cha kibiashara.