Urusi yaripoti idadi ya juu kabisa ya vifo vya COVID-19

Ujerumani imerekodi visa vipya 560 vya COVID-19 katika kipindi cha masaa 24 yaliyopita na si 741 kama ilivyoripotiwa mwanzoni, imesema taasisi ya udhibiti wa magonjwa ya Ujerumani, Robert Koch, RKI. Idadi jumla ya maambukizi hadi sasa ni 180,458.

Wataalamu wa RKI waliliambia shirika la habari la DPA kwamba takwimu za mwanzo zilikosewa kutokana na matatizo ya kiufundi, ambapo visa vya zamani vilijumlishwa na visa vipya.

Idadi ya waliokufa kutokana na virusi hivyo nchini Ujerumani haijabadilika, ikiwa ni 39 katika masaa 24 yaliyopita na kufikisha jumla ya vifo 8,450.

Nchini Urusi, hali imeendelea kuwa tete baada ya leo kuripotiwa vifo 232 idadi ambayo ni ya juu kabisa katika kipindi cha siku moja.

Mamlaka ya mji wa Moscow imetoa ripoti hiyo, ili kufifisha madai kwamba inapika takwimu. Kulingana na maafisa, watu 4,374 wamefariki nchini Urusi kutokana na COVID-19.

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Ujuwe Ugonjwa wa Busha

Kilimo cha Bamia