Uchumi wa Italia huenda ukadhoofika hadi kwa asilimia 13.

Uchumi wa Italia huenda ukanywea kwa hadi asilimia 13 mwaka huu kutokana na janga la virusi vya corona. Gavana wa benki kuu ya Italia Ignazia Visco amesema kwa kuzingatia hali ilivyo, anguko la uzalishaji kwa mwaka 2020 linaweza kuwa sawa na asilimia 9.

Onyo la Visco limekuja wakati idara ya takwimu ya taifa, Istat kutoa taarifa ya kushuka kwa makadirio ya ukuaji wa jumla wa pato la ndani la taifa, kwa robo ya kwanza.

Pato la ndani ilianguka kwa asilimia 5.3 kwa msingi wa kipindi cha robo ya mwaka, cha msimu na kalenda iliyofanyiwa marekebisho tofauti na asilimia 4.7 iliyokadiriwa Aprili 30.

Kulingana na Visco anguko hilo kwa nusu limechangiwa na hatua za kupambana na kusambaa kwa virusi vya corona na nusu nyingine imetokana na kuanguka kwa biashara ya kidunia na utalii.

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items