Na Rebeca Duwe, Tanga.
Mkuu wa wilaya ya Tanga Tobias Mwilapwa amewataka wananchi wa wilaya hiyo kuwa wamilivu kutokana hali ya ugumu wa upatikanaji wa sukuari uliojitokeza kwa kipindi hiki kwani serikali ipo kwenye mchakato wa kuleta sukari ili kuondokana na changamoto hiyo.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake kuhusiana baadhi ya wananchi kutoa kero ya ukosefu wa Sukari na baadhi ya wafanya biashara kuuza sukuari kwa bei ya juu zaidi kutokana na ukosefu huo amesema yeye kama mkuu wa wilaya amefanya utafiti na kugundua kuwa wilaya ya Tanga ina uhaba wa Sukari kwa sasa mpaka hapo serikali kuu itakapoleta sukari iliyoiahidi.
Aidha alisema baada ya kufanya msako maalumu kwenye magodown yaliyoshukiwa kuwa yangekuwa na sukari kama inadaiwa na wananchi kuwa sukari imefichwa na kwamba ndio chanzo cha kuuzwa kwa bei ghali , hivyo sio kweli kwani sukari haipo kwenye sehemu hizo.
Alisema baada uchunguzi huo ameweza kukutana na wafanyabiashara wakubwa wakiwemo wale mawakala wa sukari wilayani hapo na kueleza sababu za kutokuwepo kwa sukari kuwa ni kutokuwepo kwa uzalishaji wa sukari kwenye viwanda vya sukari hapa nchini kutokana mabadiliko ya hali ya tabia ya nchi.
Alisema mabadiliko ya hali ya hewa ya mvua iliyoendelea kunyesha ndio iliyosababisha miwa kuchelewa kukomaa hivyo imekuwa vigumu kwa viwanda kuendelea kuzalisha sukari kama ilivyozoeleka kwa miaka mingine.
Mwilapwa amesema matumaini makubwa ni serikali kuu ambayo kwa sasa imeahidi kuleta sukari ambayo imeletwa tayari nchi kiasi cha tani 4000 na kwamba tani 21000 iko njiani kwa ajili kuweza kuwasambazia wananchi kuendelea kununua sukari kwa bei ambayo serikali itaelekeza.