Wananchi wa Komarera watakiwa kupisha maeneo yalio kwenye mpango wa kuchukuliwa na Barrick



Na Timothy Itembe Mara.

MKUU wa wilaya Tarime mkoani Mara,Mtemi Msafiri amewataka wananchi na wakazi wa kijiji cha Komarera kutoendeleza maeneo yanayotakiwa kuchukuliwa na Mgodi wa North Mara Gold Mine Barrick na wala asitokee Mtu akitegesha katika eneo lolote kwasbabu kufanya hiyo ni moja ya chanzo cha  kuibua migogoro..

Akiongea mbele ya wananchi hao  kwenye mkutano wa hadhara uliokalia viwanja vya Ofisi ya serikali ya Kijiji cha Komarere alisema kuwa kuanzia leo Eneo hilo litabaki bila kuendelezwa na mtu yeyote Mgodi wa Barrick pamoja viongozi wa wa Serikali wa maeneo yenu wanaohusika kama vile wenyeviti wa vitongoji na Kijiji wataendelea kufanya mazungumzo ya Fidia.

Msafiri aliongeza kusema kuwa kwa sasa Mgodi wa Barrick umeingia Ubia na Serikali kwa hali hiyo serikali haihitaji kuona tena Mtu yeyote anaingilia zoezi hilo kwa lengo la kugomesha ama kuvuruga lisifanikiwe tunahitaji zoezi hilo kukamilika kwa wakati .na endapo atabainika Mtu yeyote akigomesha atachukuliwa hatua za kisheria.

"Sisi tumekuja kuwaarifu kuwa Eneo hili la kijiji cha Komarera Mgodi unampango wa kulichukua kwaajili ya shuguli zake Eneo ambalo Mgodi unalihitaji tunawaombeni wananchi na wale ambao walikuwa wanamiliki maeneo hayo kuanzia leo hatuhitaji tena kuona mtu anaendeleza kwa shuguli zake pisheni hadi hapo mazungumzo ya fidia yatakapokamilika"alisema Msafiri.

Mkuu wa wilaya huyo alitumia nafasi hiyo kuwaambia wananchi kuwa watu wale wabaya hawaelewa usemi huo ila wale wazuri wataelewa na kuzingatia kile serikali inachokisema.

Mdhamini mkuuwa Serikali,Evelyne Mugasha alisema kuwa hatagemei tena wananchi kuendelea kutegesha maeneo hayo swala mablo linakwamisha zoezi kutokamilika kwa urahisi na kuwa yeyote ambaye atategesha kuanzia sasa hatafanyiwa tadhimuni na kuwa hatalipwa fidia.

Kiongozi huyo alimaliza kwa kusema kuwa zoezi la udhamini na kuwalipafidia wananchi ni utekelezaji wa Rais John Pombe Magufuli alioutoa wakati kwenye ziara yake wilayani Tarime hapo mwaka 2018.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha Komarera,Nyamaganya Marwa alisema kuwa zoezi hilohalijawashirikisha wahusika kwa hali hiyo wananchi wanahitaji mazungumzo yakina ili kuridhia maeneo yaokuchukuliwa kwaajili ya shuguli za mgodi.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items