Wanawake Chalinze watakiwa kuchangamkia mikopo



Na Omary Mngindo, Lugoba.

WANAWAKE katika halmashauri ya Chalinze Bagamoyo Pwani, wametakiwa kuchangamkia fursa ya mikopo isiyokuwa na riba, inayotolewa na halmashauri yao kwa lengo la kujikwamua kiuchumi.

Rai hiyo imetolewa na Zaynabu Mkoba wa Kikundi cha Chigeze chenye makazi yake Kijiji cha Kinzagu Kata ya Lugoba wilayani hapa, akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema kuwa baadhi yao wanahofia kujiunga vikundi, hivyo kupoteza fursa hiyo ya kukopa.

Alisema kuwa baada ya kusikia uwepo wa mikopo kupitia halmashauri, waliwasiliana na ofisa anayehusika ambapo aliwapatia taratibu za kuanzisha kikundi kijulikanacho kwa jina la Chigeze, na kwamba kwa awamu ya kwanza wamepata mkopo wa shilingi milioni 3.

"Kikundi chetu kina wanachama 11, tulikianzisha mwaka 2017, tulipata mkopo wa ahilingi milioni 3 tukazirejesha ndani ya miezi 6, hivi sasa tunepatiwa mkopo mwingine wa kiasi kama hicho ambao wataendeleza bisahara za ufugaji na ukopeshaji" alisema Zaynabu.

Kwa upande wa Mwanahamisi Omary alisema kwamba wanakikundi hao sana ratiba ya kukutana kila Jumapili ambapo wanachangia shilingi elfu tano kila mmoja, kiasi ambacho kinawekwa katika akaunti ha kikundi hicho.

"Malengo yetu ya baadae ni kutafuta shamba tutalolitumia kwa kilimo ikiwa ni kuongezea mtaji wa kikundi chetu cha Chigeze, ili tuwaoneshe mfano wenzetu ambao mpaka sasa hawajakuwa na mwamko katika vikundi," alisema Mwanahamisi.

Nao Mwajuma na Hadija walieleza kwamba kutokakana na kikundi chao kuendelea vizuri na mikopo yao, wanawaomba wanawake jimboni humo na nje ya jimbo wafike kwa lengo la kujifunza namna ya kuendesha kikundi ili nao waweze kuanzisha.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items