Waziri Mkuu wa China Li Keqiang amesema leo sheria mpya kuhusu usalama wa taifa mjini Hong Kong inalenga kuimarisha uthabiti na ustawi wa muda mrefu wa mji huo.
Akizungumza baada ya kumalizika kwa vikao vya bunge mjini Beijing, Li amesema sheria hiyo tata inayowalenga kuadhibu wale wanataka kujitenga, kudhoofisha nguvu ya dola na ugaidi inanuwia kuimarisha utekelezaji wa sera ya China moja.
Wakosoaji wanasema uamuzi wa kulikwepa bunge la Hong Kong katika kupitisha sheria hiyo unaondoa misingi yote ya uhuru iliyoahidiwa na China wakati wa mkataba wa kuurejesha tena mji huo katika himaya yake mwaka 1997.