Na Thabit Madai,Zanzibar.
KADA wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Balozi Ali karume amechukua fomu ya kuwania nafasi ya Urais wa Zanzibar kupitia chama Cha Mapinduzi CCM,ambapo zoezi hilo la uchukuaji fomu limefanyika katika Ofisi kuu za chama hicho Kisiwandui Mjini Unguja.
Balozi Ali Abeid karume ni Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo Zanzibar katika Serikali ya awamu ya Saba ambaye pia ni mtoto wa muasisi Taifa Hili.
Balozi Ali karume anakuwa mtu wa Pili kuchukua fomu ya kugombania nafasi ya Urais wa Zanzibar ambapo Mbwana Bakari Juma alikuwa wa mwanzo kufika ofisini hapo na kuchukua Fomu ya kuwania nafasi hiyo ya Urais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi .
Mara baada ya kuchukua Fomu Balozi Ali Abeid karume alisema kamba iwapo chama cha Mapinduzi CCM kitampa ridhaa ya kuwa mgombea wa nafasi hiyo na kuwa Rais wa Zanzibar, anatarajia kuendelea dhamira ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuyalinda, kulinda Muungano wa Tanganiyika na Zanzibar na kuendeleza Sera za CCM.
“Iwapo nitateuliwa na chama change –CCM, na kupata Ridhaa ya Wananchi wenzangu, nategemea kuendeleza dhamira ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar kwa kuyalinda, kulinda Muungano na kuendeleza Sera za CCM” Alisema Balozi Ali Abeid Karume.
Katika Maelezo yake Balozi Ali Abeid Karume alisema kwamba Dk Ali Mohamed Shein kwa kushirkiana na Baraza la Mapinduzi amefanya kazi kubwa nay a kupigiw mfano katika kuendeleza Sera zilizoainishwa na Mzee Abeid Amani karume.
“Nia yangu ni kuyaendeleza yale yote mazuri ambayo tumeachiwa na ambayo Jemedari wa Mapinduzi yetu kama vile afya bure,Elimu bure, ugawaji wa Ardhi kwa wananchi na ujenzi wa makazi bora kwa wananchi,”alisema Balozi Ali Abeid Karume.
Aidha Balozi ali abeid Karume alisema ipo haja ya kuleta usawa wa Kijinisia, kuwalinda watoto, kuwatunza wazee na kuwwapa vijana Elimu ya kujitegemea.
“Pia pindipo nitakuwa mgombea nitakae chaguliwa na chama change na kupewa ridhaa na wananchi wa Zanzibar, Ipo haja ya kuendeleza ujamaa, udugu, upendo na mshikamano ambapo vyete hivyo ndio ngo zetu” alieleza Balozi Ali Karume.
Balozi ali Karume aliwaomba Wananchi wa Zanzibar na Makada wa chama cha Mapinduzi CCM, kumuombea kwa mwenyezimungu katika mchakato huo aliouanza pamoja na kuiombea Nchi na jamii kuwa katika hali ya Amani na utulivu.
Hii ni mara ya Pili kwa Balozi Ali Abeid Karume kuchukua fomu ya kugombania nafasi ya Urais wa Zanzibar ambapo awali alichukua mwaka 2010 ambapo Dk Ali Mohamed Shein ndie alipitishw na Chama cha Mapinduzi kuwa mgombea na kushinda kuwa Rais wa Zanzibar.
