Chama cha AAFP Waanza harakati za kuchukuo fomu kuwania nafasi ya Urais wa Zanzibar



Na Thabit Madai,Zanzibar.

PAZIA la uchukuaji wa fomu ya kuwania nafasi ya Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Wakulima (AAFP) lafungiuliwa rasmi leo ambapo Said Soud Said amekuwa mgombea wa kwanza kufika katika ofisi za chama hicho zilizopo Mwera Unguja, kuchukua fomu ya kuwania nafasi hiyo ya Urais wa Zanzibar na kuahidi kudumisha Amani na Umoja pamoja na kuenzi na kuendeleza falsafa ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya zoezi la  kuchukua fomu hiyo, Said Soud Said alisema kwamba pindipo chama chake cha Wakulima (AAFP)watampisha yeye kuwa mgombea wa Nafasi ya Urais wa Zanzibar na wananchi kumchagua atahakikisha Zanzibar anakuwa na Amani,Umoja na upendo kwa Zanzibar na watanzinia kwa ujumla.

Said Soud Said alisema pia atahakikiasha anaboresha huduma za jamii kama vile elimu bure, Afya bure, maji na salama ili kuendeleza falsafa ya Mapinduzi ya Zanzibar kama alivya asisi Hayati Abeid Amani Karume.

“Mimi nikipata ridhaa ya kuchaguliwa na Wananchi kuongoza Zanzibar, vipaumbile vyangu ni pamoja na kudumisha Amani,Umoja na upendo kwa Wazanzibar pamoja na kuboresha huduma muhimu za jamii kama vile Elimu,Afya na maji safi na salama,” alisema Said Soud Said.

Pia alisema kwamba kitu cha kwanza kukimarisha pindipo atakapochaguliwa na Wananchi ataongeza kasi ya katika ujenzi wa taifa ili maendeleo yapatikane kwa haraka na kufadika kwa wananchi wote wa Unguja na Pemba.

Alisema atahakikisha kwamba anafungua Nyanja ya vijana kupata nafasi za ajira ambapo watalipwa mishahara mikubwa ili wawe na mapenzi na taifa lao.

“Hakuna jambo kubwa ambalo Serikali hii iliyopo madarakani ambayo haijafanya, mimi nitafungua Nyanja ya vijana kupata ajira kwani vijana ndio nguvu kazi ya Taifa, vijana ndio rasilimali kubwa tunayiotegemea katika taifa hili, hivyo nitahakikisha wapata ajira na kupata mishahara mikubwa ili wasiweze kukimbia ndani ya taifa lao,”Alisema Said Soud Said.

Hata hivyo Said Soud Said alisema kwamba Serikali yake atakayoiunda atashirikisha vyama vitano vya upinzani pamoja na kuwapa mstari mbele waandishi wa habari kutokana na kazi kumbwa wanayioifanya ya kuwahabarisha umma mambo mbalimbali.

Katika Maelezo yake alisema kwamba Zanzibar inahitaji Rais mfano wa Dk Ali Mohamed Shein ambaye amefanya mazuri katika kuongoza Zanzibar ambapo amehakikisha Amani na utulivu unakuwepo wakati wote.

“Zanzibar tunahitaji Rais kama Dk Ali Mohamed Shein ambaye ni Rais mwenye busara ambapo amejitahidi kuhudumisha amani ya Nchi inaendelea kuwepo na mimi nikipata Ridhaa ntafuata nyanyo zake,”alisema Said Soud Said.

Aidha alisema kwamba pindipo Kura zake hazikukidhi kuwa Rais anaahidi kufanya kazi na Rais pamoja na Serikali ambayo itakuwa madarakani.

Nae Makamo Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima AAFP Zanzibar,  Omar Juma Said alisema kwamba Mchakato wa uchukuaji fomu ya kupata ridhaa kwa chama kuwania nafasi ya Urais wa Zanzibar umeshaanza tangu tarehe 25 na unatarajiwa kufungwa Julai 1 mwaka huu majira ya saa kumi jioni.

Alisema kwa mwananchama  yoyote mwenye sifa anakaribishwa kufika katika ofisi hizo kuchukua fomu hiyo ya kuwania nafasi ya Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya chama cha AAFP.

“Kwa nafasi hii ya Urais, mgombea anatakiwa kuwa na sifa ya kuwa Mwanachama hai,awe mtu mwenye kutambulika, awe na maadili mema ambayo anaweza kuwatumikia Wanzazbar kwa ujumla , basi huyo anaruhusiwa kuja kuchukua fomu ya Urais,” alisema Makamo mwenyekiti wa AAFP Zanzibar Omari Juma Said.

Hata hivyo alisema Chama chao kimeenza na utaratibu wa Uchukuaji wa fomu kwa nafasi ya Urais tu, hapo baadae watatoa nafasi kwa nafasi ya Uwakilishi, Ubunge na Udiwani.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items