Chama tawala Malawi chalia faulo uchaguzi wa rais, chataka kura ya tatu

Chama tawala nchini Malawi kimetoa wito wa kufanyika kwa uchaguzi wa tatu wa rais, kikielezea kasoro na vitisho wakati wa kura ya marudio iliyofanyika wiki hii, huku matokeo yasio rasmi yakionesha rais wa sasa Peter Mutharika anaelekea kushindwa na kiongozi wa upinzani.

Chama tawala cha Democratic Progressive (DPP) kimetoa wito jana Ijumaa kwa tume ya uchaguzi kufuta matokeo yaliojumuishwa mpaka sasa kutokana na uchaguzi huo wa pili na kutangaza kura ya tatu.

Matokeo yasiyo rasmi yaliokusanywa na kituo cha utangazaji cha serikali MBC yameonesha kiongozi wa upinzani Lazarus Chakwera anaongoza kwa asilimia 60, huku rais Mutharika akiwa na asilimia 39.

Katibu tawala wa chama cha DPP Francis Mphepo alisema katika taarifa kwamba kulikuwa na matukio kadhaa yenye uwezekano wa kuathiri uaminifu wa matokeo ya uchaguzi wa rais. Chama hicho kimeorodhesha vituo vya kupigia kura ambako waangalizi wake hawakushirikishwa na kusema zaidi ya kura milioni 1.5 zilikumbwa na vurugu na vitisho.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items