India na China zimekubaliana leo kutatua mzozo kuhusu eneo la mpaka ambao umezidisha misuguano kati ya mataifa hayo jirani yenye silaha za nyuklia.
Wizara ya Mambo ya nchi za nje ya India imesema katika taarifa iliyotolewa leo kuwa nchi hizo mbili zimeridhia kuendelea na mashauriano ya kidiplomasia na kijeshi huku zikihakikisha amani na utulivu vinaendelea kwenye maeneo ya mipaka.
Katika wiki za hivi karibuni mvutano kati ya China na India umeongezeka juu ya eneo la mpaka wa kiasi kilometa 3,500 uliopo kwenye jimbo la Ladakh ambao kihistoria haukugawanywa vizuri.
Maelfu ya wanajeshi kutoka kila upande wako kwenye jimbo hili na mwanzoni mwa mwezi Mei wanajeshi kadhaa wa India na china walijeruhiwa kwenye makabiliano yaliyohusisha ngumi na kurushiana mawe katika mkoa wa Sikkim.