DC Ndemanga awataka viongozi na watendaji kufanya jambo hili


Na Ahmad Mmow, Lindi.

 Mkuu wa wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga amewataka maofisa tarafa, viongozi na watendaji wa kata, mitaa, vijiji na vitongoji washiriki kikamilifu kuhamasisha wananchi wachukue tahadhari dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona.

Ndemanga amesema hayo leo,  alipozungumza na Muungwana Blog ofisini mwake, mjini Lindi.

Alisema kumekuwepo nadhana kwamba ugonjwa huo umekwisha. Hali ambayo inasababisha wananchi wengi kuacha kuchukua tahadhari, kitendo ambacho inaweza kusababisha madhara makubwa.

 Kutokana na ukweli huo, amewataka maofisa tarafa, viongozi na watendaji wa kata, vijiji, mitaa na vitongoji washiriki kikamilifu kuhamasisha wananchi wachukue tahadhari.

Aidha Ndemanga aliwataka wananchi, hasa waishio vijijini waachane na fikra kwamba ugonjwa huo upo mijini tu na umekwisha. ¥ Alisema serikali haijawahi kutangaza kwamba ugonjwa huo umekwisha. Bali maambukizi na idadi ya wagonjwa imepungua sana.

 '' Ninachoshukuru nikuona wananchi wameondokewa na hofu. Nahiyo nisilaha nzuri sana yai kushinda tatizo. Lakini sio kuacha kuchukua tahadhari,'' Ndemanga alisisitiza.

 Aidha alitoa wito kwa  asasi za kiraia, mashirika yasiyo ya kiserikali, viongozi wa dini na wanahabari waendelee kuhamasisha jamii iendelee kuchukua tahadhari.

Mkuu huyo wa wilaya licha ya kuwataka viongozi na watendaji hao washiriki na kuwajibika kikamilifu kuhamasisha wananchi kujilinda na maambukizi ya virusi vya Corona wao wenyewe wawe mfano wa kuzingatia maagizo ya serikali na wataalamu wa afya.

Alisema watendaji na viongozi hao hataeleweka na wananchi iwapo wenyewe watahubiri wasiyo yatenda. Kwani wao ni mfano wa kuigwa na wananchi.

 Alisema amebaini kwamba baadhi viongozi wa ngazi za chini hawawajibiki ipasavyo katika mapambano dhidi ya maambukizi ya Corona. Japokuwa wapo karibu na wananchi kuliko yeye, mkuu wa mkoa, waziri mkuu, makamo wa Rais na Rais na waziri wa afya.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items