Iran imesema mwanasayansi wake Sirous Asgari ambaye ni mmoja wa Wairan kadhaa wanaozuiliwa nchini Marekani, anatarajiwa kurejea nyumbani katika siku chache zijazo.
Asgari alishitakiwa na mahakama moja ya Marekani mwaka wa 2016 kwa kuiba siri za kibiashara wakati alipokuwa katiaka ziara ya elimu jimboni Ohio.
Lakini mwanasayansi huyo mwenye umri wa miaka 59 kutoka Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Sharif mjini Tehran aliondolewa mashtaka mwezi Novemba.
Msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni ya Iran, Abbas Mousavi amesema daktari huyo atarejea Iran katika siku mbili au tatu zijazo.
Wizara ya mambo ya kigeni ya Iran ilisema mwezi uliopita Asgari ameambukizwa virusi vya corona wakati akiwa kizuizini.