“Hali ya udhibiti wa corona nchini inaendelea vizuri, Tanga na Mwanza hakuna mgonjwa, pale DSM Hospitali ya Amana ina wagonjwa watatu, Mloganzila mgonjwa mmoja, Kibaha hakuna mgonjwa, nasisitiza bado Corona ipo hivyo tuendelee kuchukua tahadhari”-Waziri wa Afya Ummy Mwalimu kwenye ziara ya Waziri Mkuu Tanga leo
“Katika Uwaziri wangu sijawahi kupitia kipindi kigumu kama cha corona, kwakweli nilihenya, ila namshukuru JPM na Waziri Mkuu mlinipa nguvu, nawashukuru Viongozi wa Dini corona tumeishinda, nikiangalia Nchi nyingine nasema TZ tumshukuru Mungu”-WAZIRI UMMY
