Na Ezekiel Mtonyole, Dodoma.
Ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali hasa kipindi hiki imeruhusu vyuo na shule za za sekondari kwa kidato cha sita Mbunge wa Dodoma Mjini kupitia chama cha Mapinduzi (CCM) Anthony Mavunde, amekabidhi vifaa kinga kwa shule zote zenye kidato cha sita katika jiji la Dodoma ikiwa ni ndoo na sabuni kwa shule zote za serikali na zile za binafsi.
Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa hivyo Mbunge huyo amesema lengo la kukabidhi vifaa hivyo ni kuhakikisha wanafunzi wanasoma katika mazingira salama hasa kipindi hiki wametoka likizo ndefu na wanakaribia kufanya mitihani yao ya mwisho.
“Vifaa hivi natoa kwa shule zote zenye kidato cha sita zile za serikali na za binafsi ni kuhakikisha wanafunzi wanakuwa salama mda wote wawapo shuleni
“Na vifaa hivi nitakabidhi kwa kila mwalimu mkuu ambapo nitamkabidhi ndoo kubwa(jaba) yenye uwezo wa kuhifadhi maji mengi na ndoo za kawaida nne na sabuni ambazo zitawekwa mahali tofauti katika shule zetu” amesema Mhe. Mavunde.
Amesema amesukumwa kufanya hivyo ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali katika kupambana na ugonjwa huo, na amewataka wanafunzi wanaorudi shuleni kuzingatia masoma ikiwa ni pamoja na kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa corona ili wamalize mitihani yao salama kabisa.
Amewataka kusoma kwa bidii ili wafaulu vizuri na kuiletea sifa nzuri jiji la Dodoma na ukizingatia ndio makao makuu ya chama na serikali na wao kama viongozi katika nafasi yao watafanya kila njia kuhakikisha wanafunzi wanasoma katika mazingira mazuri.
Kwa upande wake afisa elimu sekondari jiji la Dodoma Bi Upendo Rweyemamu, ameshukuru kupatiwa msaada huo kwa shule zake na kusema itakuwa msaada mkubwa katika kipindi hiki shule zinafunguliwa.
“Ni mshukuru mhe. Mbunge amekuwa msaada sana kwa jamii yake katika jiji la Dodoma na sio leo tu tumekuwa tukishirikiana mara kwa mara na msaada huu utaenda kuwa saidia sana wanafunzi kusoma katika mazingira mazuri” amesema Upendo.
Nae mwakilishi wa wakuu wa shule zenye kidato cha sita kwa jiji la Dodoma Mwalimu Lowael Lyimo, ambaye ni mkuu wa shule ya Maria De Mathias, amemshukuru Mbunge huyo kwa mchango wake katika sekta ya elimu kwa shule zote kwani mda wote amekuwa msaada kuziwezesha shule na hata kuwapa nasaha wanafunzi pindi anapotembelea shuleni.
