Miji ya New York na Chicago nchini Marekani imeondoa amri ya kutotembea nje, kufuatia maandamano ya mwishoni mwa wiki ya kupinga ubaguzi wa rangi na ukatili unaofanywa na polisi.
Maandamano ya amani yaliendelea jana mjini New York huku maelfu ya waandamanaji wakifurika katika mtaa wa Manhattan. Wakati huo huo, maelfu ya watu walimiminika katika miji mbalimbali ya UIaya kuonyesha mshikamano wao kwa vuguvugu la kupinga ubaguzi dhidi ya watu weusi kufuatia kifo cha George Floyd, Mmarekani mweusi aliyeuawa mikononi mwa polisi.
Katika bandari ya Bristol nchini Uingereza waandamanaji walivunja sanamu la karne ya 17 la mfanyabiashara wa utumwa Edward Colston. Maandamano pia yalishuhudiwa mjini Brussels, London, Cologne, Bonn, Stuttgart miongoni mwa miji mingine.
Floyd, aliuawa akiwa amefungwa pingu wakati polisi mzungu wa mjini Minneapolis, alipogandamiza goti lake katika shingo yake kwa takriban dakika tisa hata baada ya kusema kuwa hawezi kupumua
