Mwanaume akamatwa Ujerumani akitishia kuwashambulia Waislamu


Mwanaume mmoja amekamatwa nchini Ujerumani baada ya kudaiwa kutishia kuwashambulia Waislamu, akitolea mfano mshambuliaji aliyeushambulia msikiti wa New Zealand mwaka uliopita.

Waendesha mashtaka wamesema leo kuwa mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 21 kutoka mji wa Hildesheim, anatuhumiwa kwa kutangaza nia yake kwenye mtandao wa intaneti siku ya Ijumaa ya kufanya shambulizi hilo na kuwaua watu wengi.

Mtuhumiwa huyo alikamatwa Jumamosi iliyopita na wapelelezi walikuta silaha nyumbani kwake pamoja na nyaraka zenye maelezo kuhusu matawi ya itikadi kali za mrengo wa kulia.

 Jaji ameamuru mtu huyo aendelee kuwekwa kizuizini kwa tuhuma za kuvuruga amani kwa kutishia kufanya uhalifu na kufadhili ugaidi, kosa ambalo waendesha mashtaka amesema linatokana na silaha zilizokutwa nyumbani kwake.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items