Rais Magufuli Apiga simu na kumpa mkandarasi Maagizo haya.

Na Ahmad Mmow, Ruangwa.
Katika hali inayodhihirisha Rais Dkt John Magufuli hataki ubabaishaji na ubadhirifu katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Leo amepiga simu na kuagiza mkandarasi aliyeteuliwa kujenga barabara ya Nanganga-Ruangwa, China Railways 15 Group Corporation akamilishe ujenzi kwawakati, kwa kiwango bora na azingatie thamani ya fedha.

Rais Magufuli alitoa agizo hilo kwa njia ya simu wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba wa ujenzi huo wa barabara kwa kiwango cha lami. Hafla ambayo ilifanyika mjini Ruangwa.

Rais Mgufuli alisema ujenzi wa barabara hiyo ni miongoni mwa utekelezaji wa ahadi alizohaidi kwa wananchi wa Ruangwa wakati anaomba kura kwa wananchi wawilaya na jimbo la Ruangwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Kwakuzingatia ukweli huo, Rais amemtaka mkandarasi azingatie muda kwa kukamilisha ujenzi huo kwa mujibu wa mkataba, kwakiwango bora na thamani ya fedha.

 '' Nina matuini kuwa ujenzi wa barabara  hiyo utajengwa kwa wakati na utazingatia thamani ya fedha,'' alisisitiza Rais Dkt Magufuli.

Kwaupande wake mkurugenzi mkuu wa wakala wa barabara (TANROADS), Mhandisi Patric Mfugale alise tangazo la ujenziwa barabara hiyo lilitolewa tarehe 19 Machi 2020. Ambapo wakandarasi 13 waliomba kupewa kandarasi.

Hatahivyo kampuni hiyo ya China Railways 15 Bureau corporation ndiyo ilishinda zabuni. Mhandisi Mfugale alisema ujenzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilo meta 53.2  ni miongoni mwa barabara muhimu kiuchumi katika mkoa wa Lindi. Kwani inaunganishwa na mkoa wa Mtwara ambao ni jirani wa mkoa huu wa Lindi.

Ujenzi wa barabara hiyo muhimu kiuchumi hadi kumalizika kwa mujibu wa mkataba huo uliosainiwa leo utagharimu shilingi 59.2 bilioni. 
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items