Rapa T.I apata shavu la kufundisha muziki wa Trap chuo kikuu Atlanta

Rapa T.I ameripotiwa kuwa yupo mbioni kuanza kufundisha somo la biashara ya muziki wa Trap kwenye Chuo Kikuu cha Clark Atlanta nchini Marekani.

T.I anatajwa kupata nafasi hiyo kutokana na mafanikio yake makubwa aliyoyapata katika muziki huo na atashirikiana na Daktari Mashuhuri wa maswala ya Muziki Dr. Melva K. Williams katika kufundisha somo hilo “Business of Trap Music.” kwa wanafunzi wa shahada ya kwanza wa chuo hicho.
-
"Nina furaha sana kupata nafasi ya kuonyesha uelewa wangu kuhusu #Trap ambao utavisaidia vizazi vijavyo. Muziki wa Trap umekua ni moja ya Muziki wenye Nguvu zaidi duniani na kuwa ni moja ya utamaduni wa mtu mweusi" alisema T.I baada ya kupata nafasi hiyo.

Kuhusu Trap: Huu ni miongoni mwa aina ya muziki wa Hip Hop unaofanya vizuri kwa sasa.

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items