Polisi mjini Hong Kong imekataa kutoa ruhusa ya kufanyika maandamno ya kila mwaka kuadhimisha eneo hilo kutoka kwenye mikono ya wakoloni wa zamani, Uingereza ambayo hufanyika kila Julai mosi. Mnamo mwaka 1997 mji wa Hong Kong ulirudishwa mikononi mwa China.
Katika notisi kwa mratibu wa maandamano hayo na makundi ya Haki za Binadamu, idara ya polisi imesema inazingatia sheria ya sasa ya jiji hilo inayozuia mikusanyiko ya zaidi ya watu 50 kwa sababu ya janga la corona.
Hatua hiyo imechukuliwa kabla ya mkutano wa siku tatu wa Bunge la China utakaoanza hapo kesho Jumapili ambapo Bunge linatarajiwa kuidhinisha sheria mpya ya usalama wa kitaifa.