https://monetag.com/?ref_id=TTIb Uchunguzi binafsi wabaini George Floyd alikufa kwa kukosa hewa | Muungwana BLOG

Uchunguzi binafsi wabaini George Floyd alikufa kwa kukosa hewa


George Floyd, raia mweusi wa Marekani ambaye kifo chake kimesababisha maandamano makubwa Marekani, alikufa kutokana na ukosefu wa hewa safi ya (oksijeni), kwa mujibu wa uchunguzi binafsi wa maiti yake.

Alifariki kwa kukandamizwa kwa goti shingoni na mgongoni na maafisa wa polisi wa Minneapolis, uchunguzi wa kimatibabu uliosimamiwa na familia ya Floyd umebaini hilo.

Matokeo hayo yanatofautiana na matokeo ya uchunguzi wa mwili wake uliofanywa na madktari wa kaunti.

Kulingana na matokeo hayo, hakukupatikana ushahidi wowote unaohusisha ukosefu wa hewa wala kunyongwa.

Matokeo ya uchunguzi huo wa kimatibabu pia yalibaini kwamba matatizo ya afya yalichangia pakubwa kifo cha Bwana Floyd.

George Floyd: Dakika 30 za mwisho kabla ya kifo chake
Lakini madaktari waliosimamiwa na familia ya Floyd walibaini kwamba kifo chake kilikuwa ni mauaji, taarifa kutoka kwa timu yake ya sheria inasema.

"Sababu ya kifo kwa maoni yangu kimesababishwa na ukosefu wa hewa, kutokana na kukandamizwa shingoni ambako kunaweza kutatiza oksijeni inayokwenda kwenye ubongo - na kupelekea mkandamizo mgongoni, ambako kuna tatiza upumuaji," Dkt. Michael Baden, aliyekuwa daktari wa mji wa New York pamoja na mwengine wamesema katika mkutano na wanahabari.

Haki miliki ya pichaAFP
Video inayoonesha afisa wa polisi mzungu akiendelea kupiga goti juu ya shingo ya George Floyd hata baada ya kusema kwamba anashindwa kupumua imesababisha hasira na ghadhabu miongoni mwa raia tangu ilipoonekana wiki moja iliyopita.

Tukio hilo limesababisha maandamano ya siku sita mfululizo kote Marekani na machafuko ambayo hayajawahi kushuhudiwa kwa miongo kadhaa katika maeneo mbalimbali nchini humo.

Benjamin Crump, wakili wa familia Floyd, Jumatatu amesema katika mkutano na wanahabari:

''Bila shaka leo hii leo angekuwa hai ikiwa hangekumbana na shinikizo ya namna ile kwenye shingo yake kuliko sababishwa na Derek Chauvin aliyekuwa afisa wa polisi pamoja na mvutano uliotokea kutoka kwa maafisa wengine wawili."

Aliongeza kwamba: " Ambulansi ilikuwa gari ya kubeba maiti yake."

Dkt. Baden anasema hakuwa na tatizo jingine lolote la afya ambalo huenda lingesababisha au kuchangia kutokea kwa kifo chake".