Umoja wa Mataifa watimiza miaka 75 tangu kuundwa

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema migogoro duniani inazidi kuendelea na kwamba huo ndio ukweli unaotukabili. Guterres ameyasema hayo katika kuadhimisha miaka 75 tangu kuundwa kwa taasisi hiyo.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema watu wanazidi kupoteza imani juu ya serkali zao na ameonya juu ya siasa za kujitenga zinazotishia ushirikiano wa kimataifa. Guterres ameshutumu ubaguzi wa rangi, hamaki na chuki dhidi ya wageni.

Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amesema maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi yanayofanyika sasa yalitanguliwa na harakati za kupinga tofauti katika hali za maisha na kupinga ubaguzi pamoja na ukosefu wa fursa sawa.

Katika hotuba yake bwana Guterres pia amezungumzia masuala ya msingi juu ya ubaguzi, mabadiliko ya tabia nchi, vita vya kimtandao, hujuma dhidi ya haki za binadamu na juu ya hatari ya kuzuka janga lingine la afya. Guterres amesisitiza juu ya umuhimu wa ushirikiano wa dunia.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items