Urusi kuondoa vizuizi vya kuzuia kusambaa kwa COVID-19

Urusi imetangaza kuwa itaondoa hatua kadhaa zilizowekwa ili kuzuia kusambaa kwa virusi vya corona, ikiwemo masharti makali yaliyowekwa Moscow, licha ya nchi hiyo kuendelea kurekodi maelfu ya maambukizi mapya kila siku.

Meya wa Moscow, Sergei Sobyanin amesema marufuku hiyo itamazilika kesho, ambapo wakaazi wa mji huo wataruhusiwa kutembea kwa mara ya kwanza tangu mwishoni mwa mwezi Machi.

Nchini Uingereza, idadi ya watu waliokufa kutokana na ugonjwa wa COVID-19 imefikia 40,597 baada ya kurekodiwa vifo 55 hapo jana.

Takwimu hizo za serikali zimechapishwa leo. Utafiti mpya umeonyesha kuwa hatua kali zilizowekwa na nchi za Ulaya kuzuia kusambaa kwa virusi vya corona, huenda zimezuia zaidi ya vifo milioni tatu.

Watafiti katika Chuo cha Imperial cha London, wamezingatia vizuizi vilivyowekwa kwenye nchi 11 za Ulaya. Zaidi ya watu 400,000 wamekufa kutokana na COVID-19 na zaidi ya milioni saba wameambukizwa.

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia