Boris Johnson hatokubali kuwepo ubaguzi Uingereza

Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson hatokubali kwamba nchi hiyo ni ya kibaguzi, lakini anakiri kuwa bado kuna mambo yanayopaswa kufanywa ili kupambana na visa vya ubaguzi.

Akizungumza leo na waandishi habari, msemaji wa Johnson amesema waziri mkuu huyo wa Uingereza bila shaka anaona bado kuna ubaguzi, lakini hakubaliani kwamba Uingereza ni nchi ya kibaguzi.

Amesema Uingereza imepiga hatua katika suala hilo na kwamba Johnson ana nia thabiti ya kuendeleza juhudi za kukomesha kabisa ubaguzi.

Wakati huo huo, serikali ya Ufaransa inajitahidi kushughulikia hofu inayoongezeka kuhusu ghasia zinazofanywa na polisi na ubaguzi ndani ya jeshi la polisi, wakati ambapo maandamano ya kupinga mauaji ya George Floyd nchini Marekani yakizusha hasira duniani kote.

Waziri wa Mambo ya ndani wa Ufaransa, Christophe Castaner anafanya leo mkutano na waandishi habari, baada ya maandamano yanayohusiana na mauaji ya Floyd kufanyika kwenye miji ya Ufaransa.

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia