Matumizi ya samaki yaongezeka duniani

Umoja wa Mataifa umesema watu zaidi wanakula samaki, ikionyesha ukweli kwamba matumizi ya samaki yameongezeka mwaka 2018 hadi kiwango cha juu cha kilo 20.5 kwa kila mtu. Shirika la Chakula na Kilimo Duniani, FAO limesema takwimu hizo zinaweza kuongezeka zaidi katika muongo ujao na kusisitiza jukumu muhimu la usalama wa chakula na lishe.

Hayo yamo kwenye toleo la mwaka 2020 la FAO kuhusu Hali ya Uvuvi na Kilimo Duniani. Shirika hilo limeziorodhesha Bangladesh, Cambodia, Gambia, Ghana, Indonesia, Sierra Leone, Sri Lanka na visiwa vidogo kama nchi zinazotegemea zaidi samaki.

Takriban tani milioni 179 za samaki ziliuzwa duniani mwaka 2018, huku tani milioni 156 zikiwa kwa ajili matumizi ya binadamu na asilimia 46 zilitokana na ufugaji wa samaki.

Kwa mujibu wa FAO, China ndiyo muuzaji mkubwa wa samaki.

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia