Uturuki yatoa msaada wa Barakoa kwa Brazil

Uturuki imetoa msaada wa barakoa kwa Brazil, nchi iliyoathirika kwa kiasi kikubwa na maambukizi ya virusi vya Corona.

Kulingana na taarifa iliyoandikwa kutoka kwa Balozi Mkuu wa Uturuki huko Sao Paulo,  Uturuki imetoa msaada wa barakoa zitakazosaidia katika moja ya hospitali mjini humo.

Kwa mujibu wa habari, Uturuki imetoa msaada huo kama ishara ya mshikamano wa kimataifa na kuiunga mkono nchini ya Brazil katika wakati huu ambapo nchi hiyo imeathiriwa vibaya na maambukizi ya virusi vya Corona.

Mji wa Sao Paulo ni kituo cha biashara cha nchi hiyo na ndio mji uliokuwa na watu wengi zaidi Brazil, Brazil ni kati ya nchi zilizoathirika kwa kiasi kikubwa na ugonjwa wa Covid-19.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items