Wiki mbili baada ya kifo cha mmarekani mweusi George Floyd wabunge wa chama cha democrats wanatarajiwa kuwasilisha bungeni muswada wa sheria wa kukomesha ukatili wa polisi na ubaguzi wa rangi.
Kesho Jumatatu kundi la wabunge kutoka jamii ya watu weusi lenye zaidi ya wajumbe 50 katika Baraza la Wawakilishi na Seneti wataongoza juhudi hiyo mpya inayonuwia kukomesha matumizi ya nguvu na mbinu za kikatili zinazotumiwa na polisi hususan dhidi ya watu weusi nchini Marekani.
Sheria hiyo inayolenga pia kuanzisha utunzaji kumbukumbu wa matendo ya polisi yanayokiuka maadili inaungwa mkono na viongozi wa juu wa chama cha Democratic akiwemo spika Nancy Pelosi na kiongozi wa wademocrats katika Baraza la seneti Chuck Schumer.
Hata hivyo wabunge hao watahitaji msukumo mkubwa kutoka ndani na nje ya bunge kuweza kupitisha sheria hiyo mbele ya baraza la seneti linalodhibitiwa na chama cha Rebuplican ambacho kiongozi wake wa seneti amesema haoni umuhimu wa kuwepo sheria hiyo.