WHO yaunga mkono maandamano ya kupinga ubaguzi nchini Marekani


Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kwamba, linaunga mkono maandamano yanayofanyika kote dunia kupinga ubaguzi wa rangi.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani, Tedros Adhanom amesema kuwa, anaunga mkono usawa baina ya wanadamu na vilevile harakati ya dunia nzima ya kupinga ubaguzi wa rangi.

Tedros Adhanom pia amewataka waandamanaji kote duniani kutilia maanani taratibu zote za usalama wa afya ikiwa ni pamoja na kuvaa barakoa, kuosha mikono yao kwa sabuni na kuheshimu sheria za kipindi hiki cha maambukizi ya corona. Mkuruugenzi Mkuu wa WHO ameongeza kuwa, shirika hilo linapinga aina zote za ubaguzi wa rangi.


Miji ya nchi mbalimbali duniani inaendelea kushuhudia maandamano makubwa ya watu wanaopinga ubaguzi wa rangi chini ya kaulimbiu ya "maisha ya watu weusi yana umuhimu".

Harakati hiyo ya dunia nzima ya kupinga ubaguzi wa rangi ilianza baada ya polisi mzungu wa Marekani kumuua kikatili raia mweusi wa nchi hiyo, George Floyd hapo tarehe 25 Mei katika mji wa Minneapolis jimboni Minnesota nchini Marekani. 
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items